Duration 27:23

Jinsi Nilivyotumia Mtandao Wa Facebook na Instagram Kutengeneza Hadi Tshs. 945,000 Kwa Siku

13 866 watched
0
191
Published 6 Oct 2017

Nenda https://goo.gl/6VeFGr kupata OFA yako Hongera na karibu katika mafunzo mafupi ya "Jinsi ya kutumia mtandao wa Facebook na Instagram Kunasa Wateja" Ndani mafunzo haya utapata kujifunza njia tunazotumia kutengeneza hadi Tshs. 990,000 kwa siku kupitia mtandao wa Facebook na Instagram na jinsi tulivyoweza kufanya hivyo bila ya kutumia mitandao hiyo mara kwa mara, wala kuwa na likes nyingi au followers wengi. Lakini kabla sijaanza kukuonyesha SIRI ya mafanikio yetu, inabidi niwe muwazi kwa kukwambia kuwa njia hizo tunayotumia kupata mafanikio hayo japokuwa si ngumu, sio kwa ajili ya kila mtu. Kama una nia ya kutumia njia hizo kwa lengo la kutengeneza pesa tu na sio kwa nia safi ya kutatua matatizo ya wateja wako basi mafunzo haya si kwa ajili yako. Kama wewe ni dizaini ya mtu mwenye kutaka kutengeneza pesa kiurahisi bila ya kuhangaika (get rich quick) mafunzo haya si kwa ajili yako. Kama bidhaa/huduma unazouza ni mbaya na hazipendwi na wateja wako basi mafunzo haya vile vile si kwa ajili yako. Mafunzo haya ni kwa ajili ya wajasiriamali wenye nia safi ya kutaka kutatua matatizo ya wateja wao watarajiwa au kuwapa kitu wanachokaka kupitia bidhaa/huduma zao. Kama huyo ndio wewe basi hongera! Utajifunza mambo mazito yatakayobadilisha biashara yako kwa kiasi kikubwa. Na haijalisha kama wewe unauza bidhaa zenye chapa binafsi (physical branded products), unatoa huduma za kitaalamu (expert services) kama mahesabu (accounting), huduma za kiafya (health & wellness) au ni tu wa kati kama dalali (agent) au Network Marketer. Formula utakayojifunza leo inafanya kazi kwa biashara aina nyingi tofauti. Lakini kabla sijaingia kwenye mafunzo na kukuonyesha formula hii itakuwa vizuri ukanifahamu mimi ni nani na kwanini uyape uzito maneno yangu. Kwa jina naitwa Dr. Said Said. Ni Mkurugenzi wa kampuni iitwayo Online Profits, kampuni inayowasaidia wajasiriamali wa kiAfrika kupata wateja kupitia mtandao wa intaneti. Mbali na kutoa huduma hizo kwa wajasiriamali, vile vile ni mwandishi wa vitabu na makala ndani nan je ya mtandao. Makala yangu yameonekana katika magazeti kama Daily News, Arusha Times, Man Magazine na Business Times. Japokuwa kitaaluma ni daktari wa binaadamu nimekuwa mjasiriamali wa mtandao kwa zaidi ya miaka 7. Nikisema mjasiriamali wa mtandao ninamaanisha kuwa nimekuwa nikitumia mtandao wa intaneti katika biashara zangu kupata zaidia ya 80% ya wateja. Yaani badala ya kuwatafuta wateja hao ana kwa ana, au kuweka matangazo kwenye TV, radio au magazeti (japokuwa hufanya hivyo baadhi ya wakati), jukwa maalum niliochagua kunasa wateja ni mtandao wa intaneti hususan Facebook, Instagram na hata WhatsApp. Lakini mambo hayakuwa hivyo nilivyoanza. Nilivyoanzisha kampuni yangu ya kwanza yenye kuwatengenezea wajasiriamali tovuti za kisasa, nilikuwa nikikutana na wateja wangu watarajiwa ana kwa ana kwa kuanza kuwapa ushauri bure namna wanavyoweza kutumia mtandao wa intaneti kupata wateja. Ushauri wangu ulikuwa ukipendwa sana kiasi ambacho walijenga uaminifu kwangu na kuwa tayari kuwa wateja wangu japokuwa sikuwa na vyeti vyenye kuthibitisha taaluma yangu ya kutengeneza tovuti hizo. Japokuwa mimi ni mtu mwenye haya, nilikuwa nikipata mafanikio kiasi fulani kupitia njia hiyo kwani niliweza kuonyesha upekee wa huduma zetu na kulikuwa na watu wachache waliokuwa wakitoa huduma ninazotoa. Ila changamoto kubwa iliyonikabili mimi na kampuni yangu nikuwa wafanyakazi wangu walishindwa kufanya ninayofanya na baada ya wateja kuongezeka sikuwa napata muda wa kukutana na watu ana kwa ana jambo ambalo lilifanya mauzo mapya kupotea. Hapo ndipo nilipoamua kuzama kwenye mtandao wa intaneti na kutafuta njia mbadala na kuamua kuchagua Facebook kuwa jukwa letu jibya la kupata wateja kwa sababu zifuatazo: 1. Facebook ni mtandao yenye watumiaji wengi kuliko mtandao wowote (zaidi ya Bilioni moja duniani) 2. Watu walikuwa wakitumia muda mwingi kwenye mtandao wa Facebook kuliko mitandao mengine. 3. Facebook ndio mtandao wenye kuwafahamu wateja wangu watarajiwa wanaotumia mtandao wao pamoja na sifa na mienendo zao. 4. Kasi ya ukuwaji wa mtandao huo ulikuwa ni mkubwa mno. 5. Gharama za kulipia kwenye mtandao huo ni ndogo mno ukilinganisha na mitandao mingi. Ki ufupi mtandao wa Facebook (na Instagram) ndio imekuwa TV, radio na gazeti mpya na waTanzania wengi wanahamia huko. Na sehemu yoyote yenye watu wengi, fursa ya pesa inakuwa kubwa.

Category

Show more

Comments - 22