Duration 1:14

BAJETI YAMUIBUA RUNGWE/AMSHANGAA SPIKA NDUGAI

1 786 watched
0
10
Published 24 Jun 2021

MWENYEKITI wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe, amestaajabishwa na hatua ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kushangilia Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2021/22, ya Sh. 36.3 trilioni, kupitishwa bila kupingwa bungeni. Bajeti hiyo ilipitishwa jana tarehe 23 Juni 2021, bungeni jijini Dodoma, kwa kura za ndiyo 361 (94%), kati ya 385 za wabunge walioshiriki zoezi hilo, huku 23 (6%) zikiwa ni kura zisizokuwa na upande ‘Abstain’. Kura za hapana hazikuwepo. Akizungumza na MwanaHALISI TV leo tarehe 23 Juni 2021, ofisini kwake Makumbusho jijini Dar es Salaam, Rungwe amesema, Spika Ndugai hakupaswa kushangilia kitendo hicho, kwa kuwa kilitarajiwa kufanyika, kwani Bunge hilo lina asilimia kubwa ya wabunge wa Chama tawala Cha Mapinduzi (CCM). “Spika mwenyewe ndiyo unamuona hivyo, yeye yuko pale anasifia mimi sijawahi kuona. Wewe hujawahi kuona wakati unajua wabunge wote wa CCM, we hujawahi kuona kitu gani? Ungeshangaa kama wabunge asilimia kubwa sio wa CCM na wote wamepiga kura, lakini vinginevyo ni mtu anayestajaabisha,” amesema Rungwe. 🔘JE, NA WEWE UNA HABARI? 🔘WASILIANA NA MwanaHALISI TV ( +255 767 400402), 🔘WhatsApp ( +255 692 318213) 🔘Email: mwanahalisitvnews@gmail.com 🔘KWA HABARI ZA KILA SIKU: http://mwanahalisionline.com

Category

Show more

Comments - 2