Duration 7:46

SAFARI ZA TRENI (SGR) KUANZA MWEZI WA NANE MWAKA HUU

65 338 watched
0
614
Published 14 Mar 2021

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk Leonard Chamuriho amesema safari ya reli ya Kisasa (SGR) zinatarajiwa kuanza August mwaka huu katika kipande cha Dar es salaam – Morogoro. Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua mradi huo kutoka Dodoma hadi Dar es salaam , Dk Chamuriho alisema baada ya vichwa na mabehewa ya treni kuwasili July watafanya majaribirio ya safari. Alisema ujenzi wa kipande hicho umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 huku na maeneo yaliyobaki yatakamilishwa ndani ya muda mfupi. Hata hivyo amesema katika Afrika reli ya SGR inayojengwa nchini Tanzania ndiyo bora na inaweza kuhimili mzigo mzito wa tani 35 na kubeba mabehewa mawili kwenda juu huku nchi nyingine reli yao ikiwa na uwezo wa kuhimili uzito wa tani 25. Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu Selemani Kakoso alisema wameridhishwa na ujenzi wa mradi wa treni ya mwendo kasi (SGR). Kakoso ambaye ni Mbunge wa Mpanda vijijini alisema yapo mambo ambayo wamekuwa wameishauri Serikali na tayari yamefanyiwa kazi. Alisema walikuwa wamesisitiza kuwa maeneo ambayo reli inapita wananchi walipwe haraka iwezekanavyo fidia zao ambayo jambo hilo limeshafanyiwa kazi.

Category

Show more

Comments - 176